Monday, October 12, 2015

UJERUMANI YAFUZU EURO 2016.

MABINGWA wa dunia Ujerumani, wamefanikiwa kufuzu michuano ya Euro 2016 baada ya kuichapa Georgia kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika jana. Ujerumani ilikuwa ikihitaji alama moja katika mchezo huo uliofanyika huko Leipzig ili kujihakikishia nafasi mbili za juu katika kundi D lakini bao la ushindi lililofungwa na Max Kruse dakika ya 59 liliwahakikishia kusonga mbele wakiwa vinara. Wenyeji Ujerumani ndio waliotangulia kupata bao la kuongoza lililofungwa kwa penati na Thomas Mueller kabla ya kusawazishwa dakika chache baadae na Jaba Kankava. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema wamefurahi kufuzu michuano hiyo ingawa mechi mbili za mwisho hazikumfurahisha. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa katika mechi hizo wamecheza chini ya kiwangoa chao jambo ambalo inabidi walifanyie kazi siku za mbele.

No comments:

Post a Comment