KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Xavi Hernandez amekiri angeweza kuhamia katika klabu za Manchester United au Liverpool wakati akiwa Barcelona. Mkongwe huyo alijiunga na Al Sadd kiangazi mwaka huu na kumaliza kipindi cha miaka 24 aliyoitumikia Barcelona toka akiwa mdogo. Hata hivyo, sasa amebainisha kuwa angependelea zaidi kupata uzoefu katika Ligi Kuu na kudai kuwa uhamisho wa kwenda United ungekuwa chaguo lake. Akihojiwa Xavi amesema Ligi Kuu ni kivutia kwa mchezaji yeyote kwani ni nzuri, yenye viwanja bora na mashabiki wake huwa wanaonyesha mapenzi makubwa na timu zao. Mkongwe aliendelea kudai kuwa kuna klabu nyingi kubwa zikiwemo Chelsea, United, Manchester City, Arsenal na Liverpool lakini kama angeambiwa kuchagua moja angechagua klabu yenye historia kubwa kama United au Liverpool. Xavi amesema anajua kuna klabu zimeibuka hivi karibuni kama City lakini United ndio inayomvutia zaidi kutokana na historia yake.
No comments:
Post a Comment