MENEJA wa Juventus, Massimiliano Allegri anaamini kusuasua kwa kikosi chake kumekwisha na sasa wanaweza kupamban na kutetea taji lao la Serie A. Mabao ya Alvaro Morata, Paulo Dybala na Sami Khedira yalitosha kuipa ushindi w mabao 3-1 Juventus dhidi ya Bologna jana. Ushindi huo unakuwa wa pili kwa Juventus msimu huu lakini Allegri anaamini wachezaji wake wameshaondoa hali yeyote ya uoga waliyokuwa nayo. Akihojiwa Allegri amesema mara baada ya wapinzani wao kupata bao la kuongoza wachezaji walionyesha ukomavu na kulia jambo lililowasaidia kusawazisha na kupata ushindi. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa sasa ni wakati wao wa kurejea katika ubora wao na kutetea taji lao kikamilifu.
No comments:
Post a Comment