NGULI wa zamani wa soka wa Argentina, Diego Maradona amekuwa na wikiendi ngumu kufuatia kuwa mgeni wa Radamel Falcao katika Uwanja wa Stamford Bridge juzi kabla ya kusafiri na kwenda kuitizama Argentina ikiichapa Tonga katika mchezo wa raga wa michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Uingereza. Hata hivyo matokeo hayakuwa mazuri sasa huko Stamford Bridge kwani Chelsea walichapwa mabao 3-1 na Southampton. Ushindi wa Argentina dhidi ya Tonga inaifanya timu hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya robo fainali huku wakiwa wamebaki na mchezo mmoja katika kundi lao. Maradona alionekana kirahisi katika mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Leicester City kutokana na kulele nyingi alizopiga kluishangilia nchi yake kabla ya kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo mwishoni wa mchezo na kuwapongeza wachezaji. Maradona aliwaambia wachezaji hao wa raga kuwa nchi yao yote iko nyuma yao ikiwaunga mkono wakati wote hivyo juhudi zao zitawaletea heshima ya kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment