Tuesday, October 6, 2015

HUKUMU YA EVANS KUPITIWA UPYA UINGEREZA.

HUKUMU ya kubaka ya mshambuliaji wa zamani wa Sheffield United, Ched Evans inatarajiwa kupitiwa upya na Mahakama ya Rufani nchini Uingereza kufuatia kuwasilishwa ushahidi mpya. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alihukumiwa Aprili mwaka 2012 kwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 19 katika hotel ya Rhyl kaskazini mwa Wales. Hata hivyo, Evans aliachiwa kutoka jela Octoba mwaka jana baada ya kutumikia nusu ya kifungo chake cha miaka mitano. Mawakili wa Evans wanaamini kuna baadhi baadhi ya vifungu vilikiukwa wakati wa utoaji kuhumu ya mara ya kwanza ambapo mshatakiwa alikana kufanya kosa hilo.

No comments:

Post a Comment