Tuesday, October 6, 2015

MDOMO WAMPONZA TENA MOURINHO.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho ameshitakiwa kwa kuvunja sheria na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa kauli yake kwa waamuzi kufuatia kipigo cha mabao 3-1 walichopata kutoka kwa Southampton Jumamosi iliyopita. Mourinho anadhani mwamuzi Robert Madley alikataa kuipa penati Chelsea katika mchezo huo kwasababu aliogopa kufanya hivo. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 amepewa mpaka Octoba 8 mwaka huu kujibu tuhuma zinazomkabili. Kipigo hicho kinakuwa cha nne kwa mabingwa hao watetezi wa ligi katika mechi nane walizocheza msimu huu na kuwaacha wakiwa nyuma ya vinara Manchester City kwa alama 10.

No comments:

Post a Comment