Friday, October 9, 2015

BAADA YA KUICHAPA UJERUMANI KOCHA WA IRELAND AANZA KUTAMBA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, Martin O’Neill amesema wachezaji watakwenda kutafuta ushindi wakati watakapoifuata Poland Jumapili hii kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho wa kufuzu michuano ya Euro 2016. Nchi hiyo tayari imejihakikishia nafasi ya kucheza mechi ya mtoano baada ya kufanikiwa kuwafunga mabingwa wa dunia Ujerumani kwa bao 1-0 jana lakini ushindi jijini Warsaw utawahakikishia nafasi ya kufuzu moja kwa moja. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo uliofanyika jijini Dublin, O’Neill amesema kuifunga Ujerumani ilikuwa ni juhudi kubwa zilizoonyeshwa na wachezaji wake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anajua wamepata nafasi ya kucheza mechi ya mtoano lakini Jumapili watakwenda Poland kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu muhimu.

No comments:

Post a Comment