Wednesday, October 7, 2015

KLOPP ANUKIA LIVERPOOL, KUPEWA MKATABA WA MIAKA MITATU.

KLABU ya Liverpool inakaribia kumteua meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp kuwa meneja wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu. Liverpool wanamatumaini ya kukamilisha majadiliano kesho na kumtaja meneja huyo mwenye umri wa miaka 48 raia wa Ujerumani kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers mwishoni mwa wiki. Rodgers alitimuliwa Jumapili kufuatia sare ya bao 1-1 waliyopata katika Ligi Kuu dhidi ya Everton. Klopp ametakiwa kuwachukua wasaidizi wake wa zamani Zeljko Buvaz na Peter Krawietz kuwa sehemu ya benchi lake la ufundi. Buvac raia wa Bosnia mwenye umri wa miaka 54 na Krawietz mwenye umri wa miaka 43 walikuwa sehemu watu muhimu katika benchi la ufundi la Klopp wakati akiwa Dortmund.

No comments:

Post a Comment