NGULI wan soka wa zamani wa Uholanzi, Johan Cruyff amewashukuru mashabiki wake kwa maombi yao baada ya kuthibitishwa kuwa amegundulika na maradhi ya saratani ya mapafu. Cruyff mwenye umri wa miaka 68 ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara tatu alitaarifiwa kuhusu maradhi hayo Jumanne baada ya kufanyiwa vipimo. Nguli huyo wa zamani wa klabu ya Ajax Amsterdam aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akiwashukuru wote ambao wamemtakia pole huku wakimuombea katika kipindi hiki kigumu. Mtoto wa kiume wa Cruyff ambaye alikuwa kiungo wa zamani wa Manchester United Jordi naye pia aliwashukuru watu wote ambao wamekuwa wakituma ujumbe wao wa pole. Cruyff amewahi kutinga fainali akiwa na kikosi cha Uholanzi katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1974 ambapo walifungwa na Ujerumani Magharibi.
No comments:
Post a Comment