Friday, October 2, 2015

DZEKO, SALAH WALAMBA MIKATABA YA MOJA KWA MOJA AS ROMA.

KLABU ya AS Roma imethibitisha kuwa Edin Dzeko na Mohamed Salah wamekubali kusaini mkataba wa moja kwa moja na timu hiyo. Katika taarifa iliyotolewa jana na klabu hiyo ilithibitisha kuwa wachezaji hao ambao walichukuliwa kwa mkopo wanatendelea kuitumikia timu hiyo hata baada ya msimu wa 2015-2016 wa Serie A. Dzeko na Salah walijiunga na Roma kwa mkopo wakitokea katika klabu za Manchester City na Chelsea katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi. Dzeko ambaye yuko nje kutokana na majeruhi tayari ameshafunga bao moja toka atue jijini Rome wakati Salah yeye ameshafunga mabao matatu na kuiacha timu hiyo ikishika nafasi ya sita katika msimamo wa Serie A wakiwa nyuma ya vinara Fiorentina kwa alama nne.

No comments:

Post a Comment