MSHAMBULIAJI wa Everton, Romelu Lukaku ana nia ya kufanya kazi na meneja wa Chelsea Jose Mourinho tena katika siku zijazo. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 22 alikuwa mchezaji wa Chelsea wakati Mourinho aliporejea Stamford Bridge mwaka 2013 kabla ya kupelekwa kwa mkopo Everton na baadae kuuzwa moja kwa moja. Pamoja na Mourinho kumuacha katika kikosi chake Lukaku ameonyesha kutokuwa na bifu lolote dhidi yake na angependa kufanya naye kazi siku zijazo. Akihojiwa Lukaku amesema Mourinho ni mmoja katia ya makocha ambao angependa kufanya nao kazi na baadae ndio wanakuja Arsenal Wenger na Pep Guardiola.
No comments:
Post a Comment