Friday, October 2, 2015

MWENYEKITI FA AMTAKA MOURINHO AMUOMBE RADHI CARNEIRO.

MWENYEKITI wa Chama cha Soka cha Uingereza-FA Greg Dyke amesema meneja wa Chelsea Jose Mourinho anapswa kumuomba radhi daktari wa zamani wa timu hiyo Eva Carneiro kwa kumkosoa. FA ilimsafisha Mourinho kwa kudai kuwa hakutoa kauli yeyote ya kuvunja sheria dhidi ya Carneiro lakini Dyke katika barua yake kwa wajumbe wa baraza la FA amesema Mourinho alifanya makosa. FA wamekosolewa na mmoja wa wajumbe wa bodi Heather Rabbats kwa jinsi walivyoshughulikia kesi hiyo. FA ilifanya uchunguzi baada ya mbunge mmoja kutoa malalamiko kuhusu Mourinho kutumia lugha ya kuudhi dhidi ya daktari huyo.

No comments:

Post a Comment