Tuesday, October 6, 2015

HATIMAYE TFF YAMPA SHAVU MKWASSA.

SHIRIKISHO la Soka nchini-TFF limempatia mkkataba wa kudumu kocha Charles Boniface Mkwasa kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 31, 2017. TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kuridhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria. Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka. Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.

No comments:

Post a Comment