Tuesday, October 6, 2015

RAMOS AENGULIWA KIKOSI CHA HISPANIA.

BEKI wa Real Madrid, Sergio Ramos ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kinachojiandaa kwa ajili ya mechi za kufuzu michuano ya Euro 2016. Shirikisho la Soka la Hispania lilithibitisha katika mtandao wake kuwa nacho Fernandez ameitwa kuja kuziba nafasi ya Ramos ambaye aliliripoti kambini leo kabla ya kuondoka baada ya kushauriwa na madaktari. Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 29 aliteguka bega wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk, majeruhi ambayo yalitegemewa kumuweka nje kwa zaidi ya mwezi mmoja. Akiwasili katika kambi ya timu ya taifa Ramos alidai kuwa uamuzi wa mwisho wa kama anataweza kucheza katika mechi hizo ungefanywa na madaktari wa timu. Hispania inahitaji alama moja pekee ili iweze kujihakikishia kufuzu michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Ufaransa majira ya kiangazi mwakani.

No comments:

Post a Comment