Wednesday, October 7, 2015

MAME DIOUF AWA MHANGA WA TUKIO LA MECCA.

MAMA yake mchezaji mahiri wa Stoke City, Mame Diouf ameripotiwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki katika tukio la kukanyagana wakati wakifanya Hijja huko Mecca, Saudi Arabia. Mamlaka nchini Saudi Arabia ilitoa orodha ya vifo vivyotokea huko kufikia 769 lakini vyombo vya habari vya nje na maofisa wanaripoti kuwa orodha ya watu waliokufa inazidi zaidi ya 1,000. Katika taarifa yake iliyotumwa katika mtandao klabu hiyo imesema inaungana pamoja na Diouf katika kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mtu wake wa karibu. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal ambaye pia amewahi kuitumikia Manchester Unitedalijiunga na Stoke akiwa mchezaji huru kutoka klabu ya Hannover ya Ujerumani baada ya mkataba wake kuisha Julai mwaka jana.

No comments:

Post a Comment