Wednesday, October 7, 2015

NGULI WA SOKA WA UJERUMANI ALAZWA KWA MATATIZO YA AKILI.

NGULI wa soka wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Bayern Munich, Gerg Muller amelazwa hospitali akitibiwa maradhi ya Alzheimer. Muller atayetimiza miaka 70 mwezi ujao alifunga mabao 68 katika mechi 62 kwenye kikosi cha Ujerumani ya Magharibi enzi hizo na kufunga mabao mengine zaidi 650 katika klabu. Alzheimer ni aina ya ugonjwa wa akili ambao husababisha matatizo ya kumbukumbu, kufikiria na tabia isiyoeleweka. Rais wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge alithibitisha taarifa hizo na kumtakia nguli heri ili aweze kupambana na maradhi hayo yanayomkabili na kumuahidi msaada wa hali na mali kutoka katika klabu ambayo aliijengea heshima kubwa. Muller aliwahi kushinda kiatu cha dhahabu kwa kufunga mabao 10 katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1970 huku pia akifunga bao la ushindi katika fainali ya mwaka 1974 ambapo Ujerumani ya Magharibi iliibamiza Uholanzi mabao 2-1 jijini Munich.

No comments:

Post a Comment