WAENDESHA mashitaka nchini Hispania wamefuta kesi ya kodi iliyokuwa ikimkabili mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi lakini wanatarajia kuendelea na kesi dhidi ya baba yake. Kama akihukumiwa mzee huyo aitwaye Jorge Messi anaweza kukabiliwa na kifungo cha miezi 18 jela na faini ya euro milioni mbili. Wote wawili Messi na baba yake walikuwa wakituhumiwa kwa kukwepa kodi na mamlaka nchini Hispania ya zaidi euro milioni nne. Waendesha mashitaka hao wanamtuhumu mzee huyo kwa kukwepa kulipa kodi ya mapato ya mwanaye kwa kutumia kampuni za pembeni zilizopo huko Belize na Uruguay kati ya mwaka 2007 na 2009.
No comments:
Post a Comment