MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Eden Hazard hawezi kufafanua kwanini amekuwa akicheza chini ya kiwango katika klabu yake msimu huu na kudai kuwa meneja Jose Mourinho yuko sahihi kumuondoa katika kikosi cha kwanza. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ndiye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita wakati Chelsea wakiibuka mabingwa lakini amejikuta akitemwa katika kikosi cha kwanza kutokana na kiwango kibovu alichoonyesha msimu huu. Hazard hajafunga bao lolote na amesaidia kutoa nafasi mbili pekee za mabao msimu huu na kufanya klabu hiyo kuporomoka mpaka nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi. Akihojiwa akiwa katika majukumu ya kimataifa Hazard amesema hii ni mara ya kwanza katika maisha yake amekuwa akipata wakati mgumu kwa kucheza chini ya kiwango. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa hawezi kueleza ni kwanini ila anachojua ni kwamba ataendelea kujituma kwa bidii ili aweze kurejea katika ubora wake.
No comments:
Post a Comment