BEKI mahiri wa kimataifa wa Ubelgiji, Vincent Kompany yuko fiti na anategemewa kuerejea tena uwanjani wakati timu yake ya taifa itakapocheza mechi yake ya mwisho ya kufuzu michuano ya Euro 2016 kesho. Kocha wa Ubelgiji Marc Wilmots amesema Kompany alifanya mazoezi yote bila kuonyesha kuwa na tatizo lolote na anamtegemea kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Israel. Kuitwa kwa Kompany kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu michuano hiyo dhidi ya Andorra ambao walishinda mabao 4-1 Jumamosi iliyopita na Israel utakaofanyika Brussels, kumekosolewa vikali na meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini. Pellegrini alilalamika kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa bado hayuko fiti kucheza baada ya kutoka kujiuguza majeruhi ya kigimbi ambayo yalimuweka katika mechi tano zilizopita za klabu. Hata hivyo, Wilmots amesema hajafanya mawasiliano yeyote na City lakini wamekuwa wakipewa maendeleo yake na anadhani itakuwa nzuri kwa klabu yake kama Kompany akipata mechi za kucheza.
No comments:
Post a Comment