KLABU ya Manchester City ambao walifungiwa mwaka jana na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kwa kukiuka sheri ya matumizi, wametoa faida ya mwaka kwa mara ya kwanza toka timu hiyo iliponunuliwa na Sheikh Mansour bin Zayed mwaka 2008. Klabu hiyo ya Ligi Kuu ilitoa taarifa yake ya mwaka kwa msimu wa 2014-2015 jana. Taarifa hiyo iliyotolewa imeonyesha kuwa klabu hiyo imepata faida ya paundi milioni 10.7 huku mapato yake kwa mwaka yakipanda na kufikia rekodi ya paundi milioni 352. Taarifa hiyo iliyotolewa na mwenyekiti wake Khaldoom Al Mubarak iliendelea kudai kuwa sasa City imeanza kuingiza faida huku wakiwa hawana deni lolote. Mwaka jana klabu hiyo ilitozwa faini ya paundi milioni 60 kwa kukiuka sheria hiyo ya UEFA huku pia kikosi chao kikipunguzwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment