BODI ya misamaha nchini Afrika Kusini imedai kuwa mwanariadha nyota mlemavu wa nchi hiyo, Oscar Pistorius ataachiwa kutoka gerezani na kwenda kutumikia kifungo cha nje Jumanne ijayo. Pistorius alifungwa miaka mitano jela mwaka jana baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia. Mwanariadha huyo alimfyatulia risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kupitia mlango wa bafuni akidhania kuwa ni mwizi aliyevamia nyumbani kwake. Waendesha mashitaka wamekata rufani, wakidai kuwa Pistorius alipaswa kuhukumiwa kwa kosa la mauaji na kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Novemba 3 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment