Thursday, October 1, 2015

MASCHERANO KUPANDA KIZIMBANI OCTOBA 29.

MAHAKAMA nchini Hispania imedai kuwa kiungo wa Barcelona Javier Mascherano anatarajiwa kupanda kizimbani Octoba 29 mwaka huu kujibu tuhuma za ukwepaji kodi. Jaji wa mahakama wa jiji la Barcelona alikiri kuletewa kesi na waendesha mashitaka ambao wanamtuhumu nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 31 kutumia kampuni za kigeni kuficha mapato yake halisi yanayotokana na haki ya kutumia picha zake. Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa katika kitongoji cha Gava eneo ambao Mascherano ndilo analoishi. Waendesha mashitaka wanamtuhumu kiungo huyo wa zamani wa West Ham United na Liverpool kushindwa kuweka wazi zaidi ya euro milioni 1.5 alizopata mwaka 2011 na 2012 kutokana na haki za matangazo alizotoa kwa kampuni anazomiliki Ureno na Marekani.

No comments:

Post a Comment