Thursday, October 1, 2015

MOURINHO AKWEPA KITANZI CHA FA.

MENEJA wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho hataadhibiwa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA, baada ya kuthibitika hakutumia lugha mbaya dhidi ya aliyekuwa daktari wa timu Eva Carneiro. FA ilipitia mikanda ya video iliyohusika na tukio hilo la Mourinho na Carneiro ambapo ilionekana kama alitumia lugha chafu kwa daktari huyo. Carneiro aliingia uwanjani kumtibu mshambuliaji Eden Hazard wakati wa dakika za lala salama kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Swansea, uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2. Mara baada ya mchezo na na Swansea, daktari huyo aliondolewa kuihudumia kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Carneiro amebwaga manyanga kuwepo Chelsea licha ya kutakiwa kurudi kazini na sasa yuko mbioni kusaka sheria katika mamlaka husika.

No comments:

Post a Comment