Thursday, October 1, 2015

KOCHA GUINEA-BISSAU ALIMWA ADHABU KWA KUMTUKANA MWAMUZI.

KOCHA wa timu ya taifa ya Guinea-Bissau, Paulo Torres amefungiwa kusimama katika benchi la ufundi katika mechi zilizobakia za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2017 kwa kosa la kumtukana mwamuzi. Shirikisho la Soka la Afrika-CAF lilimpata na hatia Torres ya kutumia lugha ya kuudhi na matusi kwa mamuzi aliyechezesha mechi yao dhidi ya Zambia ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana. Torres atakosa mechi ya nyumbani na ya ugenini dhidi ya Kenya Machi mwakani na kisha mechi dhidi ya Congo na Zambia. Sare hiyo ya Guinea-Bissau iliwaacha wakishika mkia katka Kundi E wakiwa wameambulia alama moja. Hata hivyo adhabu hiyo hiyo ya CAF haitaathiri mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 na Torres yuko huru kuongoza timu hiyo dhidi ya Liberia kwenye mzunguko wa kwanza.

No comments:

Post a Comment