MENEJA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema haofii chochote kuhusu kibarua chake kufuatia kuanza kwa kusuasua msimu huu. Liverpool imefanikiwa kupata ushindi katika mchezo mmoja kati ya mitano ya Ligi Kuu huku wakielekea katika mchezo mwingine mgumu dhidi ya mahasimu wao wa jiji Everton Jumapili hii. Liverpool inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi nafasi nne na alama moja nyuma ya Everton. Akihojiwa Rodgers amesema siku zote amekuwa akifanya kazi nzuri kadri awezavyo hivyo haofii chochote katika nafasi hiyo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anachozingatia ni kuangali jinsi watakavyopata alama tatu muhimu katika mchezo huo dhidi ya mahasimu wao ambao utafanyika katika Uwanja wa Goodison Park.
No comments:
Post a Comment