Sunday, October 4, 2015

LUKAKU AIPA SARE EVERTON DHIDI YA LIVERPOOL.

BADO la kusawazisha la Romelu Lukaku limeifanya Everton kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika katika Uwanja wa Goodison Park. Liverpool ndio walitangulia kupata bao la kuongoza lililofugwa kwa kichwa na Danny Ings aliyeunganisha krosi murua ya James Milner. Uokoaji mbovu wa Emre Can ulipelekea mpira kumpiga beki wa Liverpool Martin Skrtel kabla ya kuangukia kwa Lukaku ambaye hakufanya makosa na kusawazisha bao hilo. Everton sasa watakuwa wenyeji wa Manchester United katika mchezo wao unaofuata huku Liverpool wao wakifunga safari kuifuata Tottenham Hotspurs katika mchezo wao unaofuata.

No comments:

Post a Comment