KLABU ya USM Alger ya Algeria imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza pamoja na sare ya bila kufungana waliyopata dhidi ya Al Hilal ya Sudan mapema leo. USM walishinda mchezo wao wa mkondo wa kwanza kwa mabao 2-1 huko Omdurman mwishoni mwa wiki iliyopita na kufanikiwa kufuzu hatua hiyo kutokana na matokeo ya ushindi huo. Klabu hiyo sasa itaanzia nyumbani katika mchezo wa fainali ya mkondo wa kwanza inayotarajiwa kuchezwa Octoba 30 huku ile ya marudiano ikitarajiwa kuchezwa Novemba 8. USM haijawahi kufika hatua ya fainali ya michuano hiyo lakini mara ya mwisho kufanya vyema ilikuwa mwaka 2003 wakati walipotinga hatua ya nusu fainali. Katika nusu fainali nyingine TP Mazembe walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga Al Merreikh ya Sudan kwa mabao 3-0 ambayo Mtanzania Mbwana Samatta alifunga mawili. Samatta alifunga mabao hao katika dakika ya 53 na 70 huku lingine la tatu likifungwa na Roger Assale katika dakika ya 71 na kuifanya Mazembe kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2 kufuatia Al Merreikh kupata ushindi mabao 2-1 katika nusu fainali ya mkondo wa kwanza.
No comments:
Post a Comment