RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini ameungwa mkono na shirikisho hilo katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Naye rais wa Shirikisho la Soka la Asia, Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa anatarajia kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo. Platini anatuhumiwa kulipwa kiasi cha paundi milioni 1.35 na rais wa FIFA anayeondoka Sepp Blatter malipo ambayo yanadaiwa kufanyika mwaka 2011. Pamoja na kuungwa mkono huko kwa Platini, wachambuzi wa masuala ya soka wamedai kuwa nafasi yake hivi sasa inaweza kuwa mashakani kutokana na Sheikh Salman kuonyesha nia ya kugombania. Wadau hao wamesema Sheikh Salman anaungwa mkono na mataifa mengi Ulaya na duniani kwa ujumla hivyo kashfa aliyopata Platini inaweza kumuharibia kwa wajumbe kuona wamepata mbadala wake.
No comments:
Post a Comment