NCHI kadhaa zinatarajiwa kujitoa kumuunga mkono Michel Platini katika harakati zake za kutafuta nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kama hatatoa maelezo ya uhakika juu ya paundi milioni 1.35 alizolipwa na Sepp Blatter. Rais huyo wa FIFA yuko chini ya uchunguzi wa kihalifu kuhusiana na malipo hayo yaliyofanywa mwaka 2011, wakati Platini ambaye ni rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA akihojiwa kuhusiana na hilo. Wote wawili Blatter na Platini wamekanusha kufanya kosa lolote baya. Wajumbe 54 kutoka Vyama vya Soka vya nchi za Ulaya wanatarajiwa kukutana na shirikisho hilo leo nchini Uswisi kujadili suala hilo. Kukosekana kwa mkataba wa maandishi kutokana na malipo hayo kumesababisha nchi kadhaa kufikiria uamuzi wao wa kumuunga mkono Platini katika uchaguzi huo utakaofanyika Februari mwakani.
No comments:
Post a Comment