Thursday, October 15, 2015

PRINCE ALI AJITOSA RASMI KUGOMBEA URAIS FIFA.

MGOMBEA urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Prince Ali bin Hussein amepeleka rasmi maombi yake katika kinyang’anyiro hicho, akijinasibu kurejesha heshima ya shirikisho hilo baada ya hivi karibuni kukumbwa na kashfa za ufisadi. Uchaguzi huo wa kuziba nafasi ya rais aliyesimamishwa Sepp Blatter ulipangwa kufanyika Februari mwakani, ingawa mkutano wa dharura unaotarajiwa kuitishwa baadae mwezi huu unaweza kusogeza muda huo mbele. Taarifa zinadai kucheleshwa kwa uchaguzi kutatokana na kusimamishwa kwa siku tisini kwa Blatter na rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini ingawa wote wamekanusha kufanya jambo lolote baya. Hata hivyo, Prince Ali, ambaye alishindwa na Blatter katika uchaguzi wa Mei kabla ya ris huyo kutangaza kujiuzulu aliwasilisha barua yake kwa wajumbe wa mashirikisho akiomba ridhaa yao ili aweze kuitoa FIFA katika wingu zito walilopo hivi sasa. Prince Ali amesema hawataweza kubadili yaliyotokea lakini ana uhakika FIFA inaweza kuwa na mustakabali mzuri wa baadae kwa kurejesha maadili na heshima yake ya awali.

No comments:

Post a Comment