MFANYAKAZI katika danguro huko Nevada ambako nyota wa zamani wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani-NBA, Lamar Odom alipokutwa hajitambui, amewaambia wafanyakazi wa huduma ya kwanza kuwa alikuwa ametumia madawa ya kulevya aina ya Cocaine. Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Los Angeles Lakers yuko hospitali ambapo anasaidia kupumua kwa msaada wa mashine. Odom ambaye alikuwa amemuoa nyota wa luninga Khole Kardashian mwaka 2009, amekuwa akisumbuliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya kwa kipindi kirefu. Polisi wa Nevada wamesema mfanyakazi mmoja katika danguro hilo la Love Ranch alipiga simu kwa watu wa huduma ya kwanza na kudai kuwa Odom mwenye umri wa miaka 35 alikuwa ametumia Cocaine na dawa za kuongeza nguvu za kiume. Mara ya mwisho Lamar kucheza NBA ilikuwa mwaka 2013 wakati akiwa na timu ya LA Clippers.
No comments:
Post a Comment