MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Danny Welbeck ana matumaini ya kurejea uwanjani Januari baada y kukosa msimu wote mpaka sasa kutokana na majeruhi. Nyota huyo wa zamani wa Manchester United, alifanyiwa upasuaji mapema Septemba ili kutibu kabisa tatizo lililokuwa likimsumbua mwishoni mwa msimu uliopita. Welbeck amekiri imekuwa vigumu kwake kuiangalia Arsenal ikicheza akiwa nje msimu huu lakini ana uhakika wa kurejea akiwa imara zaidi baada ya kipindi cha Christmas. Nyota huyo amesema amekuwa akipita katika kipindi kigumu lakini anashukuru kidogokidogo ameanza kurejea katika hali yake ya kawaida na anamatumaini mpaka Januari atakuwa tayari amerejea uwanjani.
No comments:
Post a Comment