COCU NAYE ATOA USHUHUDA YALIYOTOKEA PARIS.
KOCHA wa klabu ya PSV Eindhoven, Phillip Cocu amebainisha kuwa alikuwepo jijini Paris Ijumaa iliyopita muda ambao magaidi walifanya mashambulizi. Zaidi ya watu 129 waliuawa katika tukio hilo la kinyama huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya katika mashabulio tofauti katika viunga vya jiji hilo. Jana mshambuliaji wa Feyenoord, Dick Kuyt alibainisha kuwa alikuwepo Disneyland Paris na familia yake wakati tukio hilo likitokea na Cocu sasa ameibuka akidai alikuwa kilometa chache kutoka eneo la tukio. Akihojiwa Cocu amesema tukio la Paris ni baya hata kulizungumzia kwani alikuwepo jijini hapo katika hoteli ambayo sio mbali sana na eneo la mashabulio. Cocu aliendelea kudai kuwa lilikuwa tukio tukio la kutisha ambalo liliwaacha watu wengi wa maeneo ya karibu wakiwa na hofu ya kutojua cha chakufanya.
No comments:
Post a Comment