KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere amesema hatafanya haraka kurejea katika kikosi cha kwanza wakati akijiandaa kurudi tena bada ya kupona majeruhi aliyopata wakati wa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya. Wilshere ambaye anategemewa kurejea katikati ya mwezi ujao mara ya mwisho kucheza mechi yake mashindano ilikuwa katika ushindi fainali ya Kombe la FA dhidi ya Aston Villa Mei 30 mwaka huu. Akiwa ameibuliwa katika kikosi cha kwanza akiwa na umri wa 16, majeruhi yamekuwa kikwazo kikubwa kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa kwani ni mara moja pekee ambayo ameshacheza mechi 25 kwa msimu mpaka sasa. Majeruhi pia yamekuwa yakimuathiri katika soka lake kimataifa akiwa ameitumikia Uingereza katik amechi 28 pekee toka alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2010. Wilshere amesema kwasasa anafanya bidii ili aweze kurejea tena uwanjani lakini hatafanya haraka mpaka hapo atapoona mwili wake unaridhia.
No comments:
Post a Comment