POLISI wenye silaha watakuwa wakifanya doria katika Uwanja wa Wembley leo wakati Uingereza itakapocheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Ufaransa siku nne baada ya mashambulio ya kigaidi jijini Paris. Stade de France, ambhapo Ufaransa ilikuwa na Ujerumani ni mojawapo ya maeneo yaliyokuwa yamelengwa na washambuliaji ambapo watu zaidi ya 129 waliouawa katika mji huo mkuu Ijumaa iliyopita. Hata hivyo, Shirikisho la Soka Ufaransa na Chama cha Soka cha Uingereza waliamua kwa pamoja kuendelea na mchezo huo jijini London huku usalama ukiimarishwa mara dufu. Zaidi ya mashabiki 70,000 wanategemewa kuhudhuria mchezo huo huku polisi wakiwataka mashabiki hao kutegemea kuwepo wana usalama wengi kuliko ilivyozoeleka.
No comments:
Post a Comment