Friday, November 20, 2015

EL CLASICO HAPATOSHI KESHO.

WINGA wa Real Madrid, Gareth Bale amesema yuko tayari kwa mapambano wakati kikosi chao kikijiandaa kwa ajili ya mchezo wa Clasico dhidi ya mahasimu wao Barcelona kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales, mwenye umri wa miaka 26, alikuwa amepata majeruhi ya nyonga Octoba mwaka huu na kukosa michezo minne kabla ya katika mchezo waliofungwa na Sevilla Novemba 8. Akihojiwa Bale amesema amekuwa majeruhi kwa wiki sita hivyo hajapata muda wa kutosha kucheza msimu huu lakini anajisikia imara na fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho. Madrid watakwenda katika mchezo huo wakiwa alama tatu nyuma ya Barcelona ambao wanaweza kuwa na mshambuliaji wao nyota Lionel Messi baada ya kupona majeruhi ya goti waliyopata Septemba mwaka huu. Messi ambaye ndio mfungaji kinara wa Clasico akiw na mabao 21, amerejea mazoezini na anaweza kurejea katika safu ya ushambuliaji ya Barcelona sambamba na nyota wenzake Luis Suarez na Neymar. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ulinzi wa hali ya juu kufuatia tukio ya mashabulio ya kigaidi ya Paris, ambapo karibu walinzi wa kujitegemea 1,500 wanatarajiwa kufanya kazi wakati wa mchezo huo wakishirikiana na polisi wapatao 1,000.

No comments:

Post a Comment