Tuesday, November 24, 2015

RAIS WA MADRID AMKINGIA KIFUA BENITEZ.

MENEJA wa Real Madrid Rafa Benitez ataendelea na kibarua cha kuinoa timu hiyo kama kawaida baada ya kuungwa mkono na rais wa klabu Florentino Perez. Shinikizo kubwa lilikuwa likimkabili kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 kufuatia kikosi chake kukubali kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa mahasimu wao Barcelona uliofanyika katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa mashabiki wa Madrid walianza kuwazomea wachezaji huku wakipunga juu vitambaa vyeupe. Akihojiwa Perez amesema walifanya kikao cha bodi na kufanya tathmini ya hali inavyoendelea katika klabu hiyo na wameamua kumuunga mkono kocha huyo na kumpa msaada wowote ataohitaji. Perez aliendelea kudai kuwa Benitez ndio kwanza ameanza kibarua hivyo wana uhakika na uwezo wake kuwa ataweza kufikia malengo waliojiwekea.

No comments:

Post a Comment