Friday, November 27, 2015

EUROPA LEAGUE ROUNDUP.

MICHUANO ya Europa League imeendelea tena jana kwa michezo mbalimbali ya hatua ya makundi kuchezwa. Miongoni mwa mechi zilizochezwa ni Liverpool waliokuwa wakicheza na Bordeaux ya Ufaransa ambapo Waingereza hao walichomoza na ushindi wa mabao wa 2-1 ambayo yamefungwa na James Milner pamoja na Christian Benteke. Ushindi huo umeifanya Liverpool kufuzu hatua ya timu 32 za michuano hiyo huku wakiwa wamebaki na mchezo mmoja mkononi. Katika michezo mingine Tottenham Hotspurs waliibugiza Qarabag ya Azerbaijan bao 1-0, Schalke 04 ya Ujerumani ikiifunga Apoel Nicocia ya Cyprus bao 1-0 huku Monaco ya Ufaransa ikiichapa Anderlecht ya Ubelgiji mabao 2-0. FC Augsburg ya Ujerumani wametandikwa mabao 3-2 dhidi ya Athletic Bilbao ya Hispania, Ajax Amsterdam ya Uholanzi imeifunga Celtic ya Scotland mabao 2-1 na FK Krasnodar ya Urusi imeiadhibu Borussia Dortmund ya Ujerumani bao 1-0. Michuano hiyo itaendelea tena December 10 kwa michezo kadhaa ambapo Fenerbache ya Uturuki itaikabili Celtic, Spurs watakuwa wenyeji wa Monaco huku FC Sion ya Uswisi wakiwakaribisha Liverpool.

No comments:

Post a Comment