Friday, November 27, 2015

COE AJITOA KUWA BALOZI WA NIKE.

RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Riadha-IAAF, Lord Coe amesitisha ushirikiano uliodumu kwa miaka 38 na kampuni kongwe ya vifaa vya michezo ya Marekani, Nike. Coe amekuwa balozi wa Nike kwa kipindi chote hicho na hatua ya kusitisha ushirikiano huo unatokana na madai ya mgongano wa kimaslahi kuhusu Eugene, Oregon kupewa uenyeji wa mashindano ta Riadha ya Dunia. Eugene, Oregon ndio yalipo makao makuu ya kampuni kubwa. Coe amesema amefikia hatua hiyo kutokana na minong’ono inayoendelea kwani haina faida kwa Nike wala IAAF. Coe pia ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kama mwneyekiti wa Chama cha Olimpiki cha Uingereza baada ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini Rio de Janeiro mwakani.

No comments:

Post a Comment