Friday, November 27, 2015

RUMMENIGGE AMPIGA KIJEMBE GUARDIOLA.

MWENYEKITI wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge jana amesisitiza kuwa hakuna mtu anayekosa mbadala kuelekea katika uamuzi wa mustakabali wa Pep Guardiola. Rummenigge amesema duniani hakuna anayekosa mbadala kwani wachezaji huja na kuondoka na hivyo pia kwa makocha. Guardiola mwenye umri wa miaka 44, yuko katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na amesema atatangaza mipango yake ya baadae na klabu hiyo kabla ya kipindi cha Christmas huku Bundesliga ikitarajiwa kusimama kupisha majira ya baridi Desemba 20 mwaka huu. Rummenigge naye alithibitisha hilo jana na kuongeza kuwa kama uamuzi wa kocha huyo utakuwa vinginevyo ana uhakika watapata kocha mwingine mzuri wa kuendeleza pale atakapoishia yeye. Guardiola ambaye ameshinda mataji 19 akiwa kama kocha kwa klabu za Barcelona na Bayern, amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment