Thursday, November 26, 2015

VANA GAAL ATAMBA KUICHAPA WOLFSBURG.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amekiri kikosi chake kinakabiliwa safari ya kwenda Wolfsburg katika mchezo wao wa mwisho wa makundi ya michuano Ligi ya Mabingwa Ulaya Desemba 8 mwaka huu lakini amejitapa kuwa watashinda na kutinga hatua ya timu 16 bora. United iko alama moja nyuma ya Wajerumani hao katika kundi lao kufuatia sare ya bila kufungana waliyopata dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi. United sasa watahitajika kushinda ili kusonga mbele kwasababu wana alama moja nyuma ya PSV wanaowafuatia ambao wana rekodi nzuri walipokutana nao. Akihojiwa Van Gaal amesema kila kitu kinawezekana na wana uwezo wa kushinda mahali popote kwani wameonyesha hilo katika Ligi Kuu na sasa wanapaswa kufanya katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment