Thursday, November 26, 2015

CHAMPIONS LEAGUE ROUNDUP.

MECHI za makundi za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zilichezwa tena jana ambapo timu 16 kutoka makundi makundi manne zilijitupa uwanjani kupigania nafasi za kufuzu hatua ya mtoano. Katika michezo hiyo timu za Real Madrid, Paris Saint-Germain, Atletico Madrid, Benfica, Juventus na Manchester City zilifanikiwa kufuzu hatua ya timu 16 bora baada ya kushinda mechi zao. Madrid wao walisonga mbele kwa kushinda mabao 4-3 dhidi ya dhidi ya Shakhtar Donesk ya Ukraine katika mchezo wa kundi A huku Paris Saint Germain nao wakisonga mbele kwa kuichapa Malmo ya Sweden kwa mabao 5-0. Hali haikuwa nzuri sana kwa timu za Uingereza jana ambapo Manchester United waling’ang’aniwa sare ya bila kufungana na PSV Eindhoven ya Uholanzi huku City wao wakipigwa bao 1-0 na Juventus. United wanaoshika nafasi ya pili katika kundi B watalazimika kushinda mchezo wao wa mwisho dhidi ya vinara wa kundi hilo Wolfsburg ya Ujerumani ili waweze kufanikiwa kufuzu huku wenzao City ambao tayari wamefuzu pamoja na kufungwa wao wakitafuta ushindi ili kumaliza vinara katika kundi D kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Borussia Moenchengladbach.

No comments:

Post a Comment