Thursday, November 26, 2015

TOURE ADAI JUVENTUS WAMEWAOTEA.

KIUNGO Yaya Toure amesema Juventus walikuwa na bahati kuifunga Manchester City mara mbili katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya mabingwa hao wa Serie A kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo huo uliofanyika jana jijini Turin. Juventus walikuwa tayari wameshawachapa City mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Manchester na kipigo cha jana kimewafanya kuporomoka mpaka nafasi ya pili katika kundi D wakiwa nyuma ya Waitaliano hao. Akihojiwa Toure amesema kiukweli Juventus wamekuwa na bahati kwani katika mechi zote mbili walikuwa na nafasi ya kusawazisha au hata kushinda kabisa. Kiungo huyo aliendelea kudai kuwa ni jambo la kuhuzunisha kwani mchezo ulikuwa unaweza ukaenda upande wowote.

No comments:

Post a Comment