Thursday, November 26, 2015

VALDES KUONDOKA MAN UNITED JANUARI.

KIPA wa Manchester United aliyetengwa Victor Valdes amesema anapambana kuwa huru kutoka katika kikosi cha timu hiyo kilicho chini ya meneja Louis va Gaal. Kipa huyo wa zamani wa Barcelona alijiunga na United akiwa mchezaji huru msimu uliopita lakini alisimamishwa na Van Gaal kwa kutokuelewana kufuatia kukataa kucheza katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21. Valdes bado anaendelea na mkataba wake Old Trafford na kutuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuwa ataendelea kujituma kwa bidii kimyakimya ili aweze kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili Januari mwakani. Valdes amesema hataki awakatishe tamaa wale ambao wanataka kumuona akicheza tena ndio maana anajituma kwa bidii huku akifurahia kazi yake hiyo.

No comments:

Post a Comment