Monday, November 30, 2015

FURY ANZA JEURI AKATAA KUZICHAPA NA HAYE.

BINGWA wa masumbwi wa uzito wa juu duniani, Tyson Fury amesema kamwe hatarajii kutetea mikanda yake ya ubingwa dhidi ya Mwingereza mwenzake David Haye. Fury aliushangaza ulimwengu wa masumbwi kwa kumtandika Wladimir Klitschko juzi na kutwaa mikanda ya WBA, IBF na WBO iliyokuwa ikishikiliwa na bondia huyo raia wa Ukraine. Lakini Fury bado hajamsamehe Haye kwa kujitoa mara mbili katika ratiba ya mapambano yao mwaka 2013 hatua ambayo anadai ilimsababishia matatizo ya kisaikologia. Akihojiwa Fury amesema kamwe hataweza kupigana na bondia huyo kwakuwa bado hajasahau alichomfanyia na kama ikitokea akilazimishwa kufanya hivyo yuko tayari kuachia mikanda yake.

No comments:

Post a Comment