Monday, November 30, 2015

KOCHA WA VALENCIA ABWAGA MANYANGA.

MENEJA wa Valencia, Nuno Espirito Santo amejiuzulu wadhifa wake huo jana baada ya kikosi chake kuchapwa bao 1-0 na Sevilla katika mchezo wa La Liga. Taarifa hizo zilivuja mitandaoni wakati mchezo bado ukiendelea na kocha huyo raia wa Ureno alithibitisha uamuzi wake katika mkutano na wana habari baada ya mchezo kumalizika. Santo alifafanua kuwa alikuwa tayari ameshaamua kuondoka klabu hap hata kabla ya mchezo huo wa jana na kuongeza kuwa wachezaji wake walikuwa hawajui kama itakuwa mechi yake ya mwisho. Kocha huyo amesema kabla ya mchezo alizungumza na rais wa klabu hiyo ambaye pia ndio mmiliki, Peter Lim na wote kukubaliana kuwa hali sio nzuri ndio maana akaamua kuondoka. Santo aliendelea kudai kuwa kikubwa anachokihitaji yeye ni klabu hiyo kufanya vyema ndio maana ameamua kuchukua uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa wengine.

No comments:

Post a Comment