Monday, November 2, 2015

GUARDIOLA ASAFIRI KWENDA BARCELONA KUMJULIA HALI SWAHIBA WAKE JOHAN CRUYFF.

MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola ametumia nafasi ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki kusafiri kwenda jijini Barcelona kumtembelea Johan Cruyff ambaye anaugua. Nguli huyo wa zamani wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 68 anaugua maradhi ya saratani ya mapafu na aliwahi kumfundisha Guardiola katika klabu ya barcelona wakati akiwa mchezaji. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Catalan, Guardiola alisafikiri kwenda nchi Hispania kukutana na Cruyff katika kitongoji cha Osona kilicho karibu na Barcelona, baada ya Bayern kutoa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Eintracht Frankfurt Ijumaa iliyopita. Hiyo inakuwa mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana toka Cruyff alipotangaza kukumbwa na maradhi hayo mwezi uliopita. Guardiola mwenye umri wa miaka 44, amekuwa akimuelezea Cruyff kama mtu aliyechangia mafanikio yake kwa kiasi kikubwa wakati akiwa mchezaji na baadae kama kocha.

No comments:

Post a Comment