Monday, November 2, 2015

KAMPUNI YA CHINA KUINUNUA ESPANYOL.

KAMPUNI ya Rastar Group ya China imetangaza leo kuwa inatarajiwa kununua asilimia 56 ya hisa katika klabu ya Espanyol ya Hispania ikiwa ni mkakati wao wa kuendelea kuwekeza katika klabu za Ulaya. Kampuni hiyo ambayo hujihusisha na biashara za magari na vipuri vyake, imesema inatarajia kulipa euro 78 kwa kila hisa katika klabu hiyo ambayo itawagharimu kiasi cha euro milioni 178. Kampuni hiyo yenye maskani yake magharibi mwa China katika mji wa Guangdong imesema itanunua hisa hizo kwa fedha taslimu. Baada ya kununua hisa hizo, Rastar imedai kuwa itaongeza uwekezaji zaidi katika klabu hiyo yenye maskani yake jijini Barcelona ambao wanashika nafasi ya 19 katika msimamo wa La Liga, kufikia euro milioni 45.

No comments:

Post a Comment