MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa ataridhika kama wakipata hata sare katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Bayern Munich Jumatano hii lakini amekiri hatakwenda kule kwa ajili ya kujilinda zaidi. Arsenal walifufua matumaini yao ya kutinga hatua ya timu 16 bora kwa ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Bayern wiki mbili zilizopita. Arsenal imeshafanikiwa kupata sare na ushindi katika Uwanja wa Allianz Arena katika safari zao mbili zilizopita walizokwenda Ujerumani. Bayern waling’ang’aniwa sare ya bila kufungana dhidi ya Eintracht Frankfurt Ijumaa iliyopita lakini Wenger amesisitiza timu hiyo bado ni hatari katika safu yao ya ushambuliaji na anaamini wakicheza kwa kujilinda sana dhidi yao wanaweza kuadhibiwa. Wenger amesema kutokana na ubora walionao katika safu yao ushambuliaji hadhani kama wataweza kujinda kwa dakika 90, hivyo la msingi ni wao pia kutoka na kushambulia.
No comments:
Post a Comment