Monday, November 2, 2015

ASTON VILLA YAPATA KOCHA MPYA.

KLABU ya Aston Villa imemteua meneja wa zamani wa klabu ya Lyon Remi Garde kuwa kocha wao mpya akichukua nafasi ya Tim Sherwood. Mfaransa huyo amepewa mkataba wa miaka mitatu na nusu na anatarajiwa kutizama mchezo wa leo akiwa jukwaani wakati Villa watakapokuwa wageni wa Tottenham Hotspurs. Garde mwenye umri wa miaka 49 anakitwaa kikosi hicho kikiwa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu wakiambulia alama nne katika michezo 10 walioyocheza. Kocha wa bastia Rigenald Ray anatarajiwa kuwa msaidizi wa Garden a kibarua chao cha kwanza kwa wawili hao kitakuwa mchezo dhidi ya Manchester City Jumapili ijayo ambao utachezwa Villa Park.

No comments:

Post a Comment